Date: 
28-02-2024
Reading: 
Mwanzo 4:9-15

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi 28.02.2024.

Mwanzo 4:9-15

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

Mawazo maovu ni chanzo cha ukatili;

Kaini na Habili walikuwa ndugu, mkulima na mchungaji wa mifugo mtawalia. Hawa wawili siku moja walileta sadaka mbele za Bwana, Kaini alileta mazao ya shamba, Habili akaleta wanyama (mifugo) iliyonona. Mungu akaitakabali sadaka ya Habili kama tunavyosoma;

Mwanzo 4:3-5

3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

Matokeo yake ilikuwa ni Kaini kumhadaa Habili waende uwandani. Kaini akamuua ndugu yake Habili.

Bila shaka kwa Bwana kutoitakabali sadaka ya Kaini kulimfanya Kaini awaze vibaya juu ya Habili, hata kumuua.

Kama torati ilivyoelekeza, na Kristo kutimiliza, kuua ni dhambi. Amri inasema usiue. Kaini aliwaza vibaya akaua. Yesu Kristo anatukumbusha kila siku kuwaza vema ili tusitende vibaya, hata kuwafanyia wenzetu ukatili. Timiza wajibu wako, ukiwaza na kutenda vema kwa Utukufu wa Mungu. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa