Date: 
27-02-2024
Reading: 
Matendo 16:29-24

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi 27.02.2024

Matendo ya Mitume 16:19-24

19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;

20 wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi;

21 tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.

22 Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.

23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.

24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.

Mawazo maovu ni chanzo cha ukatili;

Kijakazi mmoja alikuwa akifanya kazi za uaguzi, na kwa njia hii bwana zake walipata fedha nyingi. Paulo akamkemea pepo akamtoka yule kijakazi, hivyo uaguzi ukawa shida na mapato kukosekana. Sababu hii iliwafanya bwana zake yule kijakazi kuchukia, wakawakamata Paulo na Sila na kuwapeleka mbele ya wakuu wa mji wakiwashtaki kwa mafundisho yao yaliyoharibu desturi za Kiyahudi.

Paulo na Sila walipigwa bakora na kutupwa gerezani. Ukiendelea kusoma unaona wakitolewa gerezani usiku na Bwana kwa njia ya malaika wake. 

Paulo na Sila walifanyiwa ukatili pamoja na kwamba walikuwa wanahubiri Injili. Lakini wao waliendelea kumtegemea Bwana.

Tusiwatendee wenzetu vibaya, maana hilo siyo agizo la Kristo. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa