Date: 
16-01-2024
Reading: 
Mwanzo 9:1-3

Jumanne tarehe 16/01/24 asubuhi

Mwanzo 9:1-3

1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

2 Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.

Mungu habariki familia zetu

Kama vile Mungu alivyombariki Nuhu na familia yake, vivyo hivyo Mungu hubariki familia zetu tukikaa ndani yake. Ukisoma nyuma ya somo la leo, utaona Nuhu alikuwa mtiifu na mwaminifu kwa Mungu, ndipo baraka za Mungu zikaambatana nae na familia yake. Tujifunze kumwamini na kumtegemea Mungu, nasi tutabarikiwa sisi na familia zetu.

Nawatakia siku njema.

C. Swai