Date: 
26-08-2023
Reading: 
Waebrania 12:25-29

Jumamosi asubuhi tarehe 26.07.2023

Waebrania 12:25-29

25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;

26 ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

27 Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;

29 maana Mungu wetu ni moto ulao.

Tuwe wanyenyekevu;

Sura ya 12 ya waraka kwa Waebrania inawaita watu kumtazama Kristo aliye utimilifu wa imani. Mwandishi anawaita watu kuomba neema ya Mungu isiondoke kwao. 

Somo tulilosoma ni sehemu ya sura hii, mwandishi akiandika juu ya kutomkataa anenaye. Hapa mwandishi alilenga Kanisa kuwa na hamu ya kulisikiliza neno la Mungu.

Mwandishi anaendelea kusema kuwa neno la Mungu ni timilifu, na ufalme wa Mungu wadumu milele. Kwa sababu hii tunaalikwa kumfanyia Mungu ibada ya kumpendeza tukiwa wanyenyekevu mbele zake. Maisha yetu ni ibada kamili tukiwa na unyenyekevu. Amina.

Jumamosi njema 

 

Heri Buberwa