Date: 
18-08-2023
Reading: 
Luka 13:31-35

Ijumaa asubuhi tarehe 18.08.2023

Luka 13:31-35

31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.

32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.

33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.

34 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.

35 Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.

Mithali 14:34

Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Katikati ya huduma yake yenye mafundisho na uponyaji, Yesu anaambiwa aondoke na kujificha maana anatafutwa kuuawa na Herode. Yesu hakuogopa, alimuita mbweha! Akaendelea kusisitiza juu ya ujio wake duniani. Yesu anatumia maneno ya Yerusalemu kuwaua manabii akiwasema waliomkataa akiwamo Herode, kwamba watamuona Mungu watakapomkiri yeye Kristo.

Hatutakiwi kuwa waoga katika njia yetu ya ufuasi tunapomwamini Yesu. Haimaanishi tusichukue tahadhari katika kazi na maisha yetu kwa ujumla, bali tumtangulize Yesu bila kuwa waoga kama yeye alivyokuwa. Tutamuona Mungu tukidumu katika imani hii kama tulivyomkiri Kristo. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa