Date: 
25-07-2023
Reading: 
Wagalatia 4:8-10

Jumanne asubuhi tarehe 25.07.2023

Wagalatia 4:8-10

8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.

9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?

10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.

Uchaguzi wa busara;

Mtume Paulo anawakumbusha Wagalatia kuwa zamani hawakumjua Mungu, na kwa sababu hiyo waliitumikia miungu. Anawataka kutorejea mafundisho ya zamani hizo kwa sababu wamekwisha kumjua Mungu. Msisitizo wa Mtume Paulo ulikuwa kumwamini Yesu Kristo na kuachana na mafundisho ya zamani ambayo yalikuwa kinyume na Kristo.

Sisi kama kundi la waaminio tunamwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wetu aliyekufa na kufufuka, na kwa njia yake tumeokolewa. Basi tusirejee maisha ya zamani za ujinga ambayo yako kinyume na imani yetu. Tuache mafundisho yasiyofaa, tukidumu katika kumjua Mungu, sasa na siku zote. Amina.

Jumanne njema.

Heri Buberwa 

Mlutheri