Date: 
30-06-2023
Reading: 
Mathayo 15:1-9

Ijumaa asubuhi tarehe 30.06.2023

Mathayo 15:1-9

1 Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,

2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.

5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,

6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

7 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,

8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.

9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Neema ya Mungu yatuwezesha;

Mafarisayo na waandishi walimwambia Yesu kuwa wanafunzi wake waliharibu mapokeo kwa sababu walikuwa hawanawi mikono. Yesu naye akawaambia kuwa hawakushika mapokeo kwa sababu hawakuwaheshimu wazazi wao. Mafarisayo na waandishi walijihesabia haki pasipo na wao kushika mapokeo.

Mafarisayo hawakumwelewa Yesu, na kwa kutokumwelewa Yesu anawaita vipofu;

Mathayo 15:12-14

12 Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?
13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
14 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Mafarisayo na waandishi walishika mapokeo ya kale wakati walikuwa na Yesu, ndiyo maana Yesu aliwaita vipofu. Waliishika Torati bila kumwamini Yesu ndiyo maana Yesu aliwaita vipofu. Kuishika torati bila kumtazama Kristo ni kuwa kipofu, maana neema ya Mungu yatuwezesha. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa