Date: 
26-06-2023
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 31:1-5

Jumatatu asubuhi tarehe 26.06.2023

Kumbukumbu la Torati 31:1-5

1 Musa akaenda akawaambia Waisraeli maneno haya yote.

2 Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na Bwana ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani.

3 Bwana Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena.

4 Na Bwana atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na nchi yao, ambao aliwaharibu.

5 Naye Bwana atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru.

Neema ya Mungu yatuwezesha;

Musa baada ya kuambiwa na Mungu kwamba asingeingia katika nchi ya ahadi, anakuja kuwapa ujumbe huo Israeli, kwamba wataongozwa na Yoshua. Musa aliwaambia kuwa Mungu angewazuia mataifa wote ambao wangesababisha safari yao ya kurejea Kanani isifanikiwe. 

Kwa kuwahakikishia Israel kuwa safari yao ilikuwa salama, Musa anamkabidhi Yoshua uongozi;

Kumbukumbu la Torati 31:7-8

7 Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi Bwana aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
8 Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.

Hadi hapo Israeli walikuwa wanaiendea nchi ya ahadi kwa uongozi wa Yoshua, kama ilivyokuwa awali wakiwa na Musa. Yoshua aliwaongoza wakafika Kanani. 

Kristo sasa hutuongoza katika maisha yetu katika mambo yote. Kazi zetu zote hufanikiwa kwa msaada wa Yesu Kristo, ndiyo maana neema yake yatuwezesha. Amina.

Uwe na wiki njema.

 

Heri Buberwa