Date: 
17-06-2023
Reading: 
Yoshua 24:25-28

Jumamosi asubuhi tarehe 17.06.2023

Yoshua 24:25-28

25 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.

26 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana.

27 Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya Bwana aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.

28 Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake.

Mungu au Ulimwengu;

Baada ya kuwaongoza Israeli kuelekea nchi ya ahadi, Yoshua aliwaambia kuiacha miungu na kumtumikia BWANA aliyewatoa utumwani Misri. Israeli walitii na wakaahidi kumtumikia BWANA. Baada ya ahadi yao ya kumtumikia BWANA, ndipo asubuhi hii tunaona Yoshua akiweka alama ya ushahidi kwa Israeli kumtumikia BWANA, wasije kumkana na kugeukia miungu yao.

Baada ya safari ya muda mrefu, hatimaye Yoshua aliwafikisha Israeli katika nchi ya ahadi. Walikombolewa utumwani.

Haikuishia hapo.

Sisi tumekombolewa kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani pale alipoteswa na kufa kwa ajili yetu. Huyu Yesu ndiye tunayealikwa kumwamini, kumwabudu na kumtumikia daima. Tukimtumikia Yesu tunakuwa tumemchagua Mungu, na siyo Ulimwengu.

Jumamosi njema.

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 bernardina.nyamichwo@gmail.com