Date: 
05-09-2022
Reading: 
Mhubiri 5:6-8

Jumatatu asubuhi 05.09.2022

Mhubiri 5:6-8

[6]Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?

[7]Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.

[8]Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, 

Aliye juu kuliko walio juu huangalia; 

Tena wako walio juu kupita hao.

Tutumie vizuri ndimi zetu;

Somo la asubuhi hii linahusu uchaji, unyenyekevu na kuridhika. Tunasoma juu ya kusema bila kufikiri, ambapo shida huweza kutokea. Mwandishi anakemea kusema mambo ambayo mtu hana uhakika nayo, maana ni kumkosea Bwana. Ukisoma mstari mmoja kabla ya somo, anakemea kuhusu nadhiri;

Mhubiri 5:5

[5]Ni afadhali usiweke nadhiri, 
Kuliko kuiweka usiiondoe.

Juma hili tunapewa wito wa kuwa makini na maneno yetu. Tunakumbushwa kufikiri kabla ya kusema chochote. Tusiseme maneno ya kijinga kwa vinywa vyetu, wala tusiwe wepesi wa kunena, bali tuongozwe na Roho wa Mungu tukitumia ndimi zetu vizuri kwa Utukufu wake.

Uwe na wiki njema yenye matumizi mazuri ya ulimi.