Date: 
01-07-2022
Reading: 
Mathayo 24:1-4

Ijumaa asubuhi tarehe 01.07.2022

Mathayo 22:1-4

1 Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema,

2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.

3 Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja.

4 Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.

Wito wa kuingia ufalme wa Mungu;

Yesu anatoa mfano wa mfalme aliyemfanyia mwanae harusi na kualika watu ambao hawakutokea. Pamoja na kusema kuwa aliandaa vyakula na vinywaji vya kila aina, bado waalikwa walikataa kuja. Hawakujali.

Mfano huu unaakisi ambavyo Yesu anaita watu wote kumwamini na kumpokea. Anatuita kuacha vyote na kumfuata. Tusiiache neema hii kwa sababu ya mambo yanayotuzunguka. Ufalme wa Mungu unatungoja.

Siku njema.