1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Wageni waliotufikia na Cheti ni Bwana na Bibi Heri Seth Mnzava wanatoka usharika wa KKKT Kariakoo. Wanahamia hapa.
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

3. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kuwa kutakuwa na semina ya ndoa ya siku 8 kuanzia jumapili ya tarehe tarehe 24/04/2016 mpaka tarehe 01.05.2016 hapa Usharikani. Mnenaji atakuwa ni Mchungaji na Bibi Mathias Mushi kutoka KKKT Arusha. Tuendelee kuombea semina hii. Ratiba kamili itatolewa baadaye. Pia kamati ya Misioni na Uinjilisti inapenda kuwataarifu vikundi vyote hapa usharikani kwamba ile Semina ya vikundi iliyokuwa ifanyike mwezi Aprili itafanyika wiki ya tatu ya mwezi Mei. Ratiba kamili itatolewa baadaye. Aidha kamati inapenda kuwataarifu vikundi vyote kuwasilisha Ratiba za mipango yao ya mwaka huu kwa Katibu wa Kamati ya Misioni na Uinjilisti kabla ya tarehe 10.04.2016, hii ni kwa ajili ya kuweza kuainisha ratiba za mipango ya kamati ya Misioni na Uinjilisti na ya vikundi isiingiliane.

4. Kesho Jumatatu tarehe 04.04.2016 saa 11.00 jioni kutakuwa na mazoezi ya Kwaya ya Umoja kwa ajili ya maandalizi ya Kantate. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria.

5. Jumapili ijayo tarehe 10.04.2016 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae. Wazee wagawe bahasha.

6. NDOA:
Matangazo ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

Attachment: