Date: 
22-10-2019
Reading: 
John 5:10-18

TUESDAY 22ND OCTOBER 2019 MORNING                           

John 5:10-18 New International Version (NIV)

10 and so the Jewish leaders said to the man who had been healed, “It is the Sabbath; the law forbids you to carry your mat.”

11 But he replied, “The man who made me well said to me, ‘Pick up your mat and walk.’ ”

12 So they asked him, “Who is this fellow who told you to pick it up and walk?”

13 The man who was healed had no idea who it was, for Jesus had slipped away into the crowd that was there.

14 Later Jesus found him at the temple and said to him, “See, you are well again. Stop sinning or something worse may happen to you.” 15 The man went away and told the Jewish leaders that it was Jesus who had made him well.

The Authority of the Son

16 So, because Jesus was doing these things on the Sabbath, the Jewish leaders began to persecute him. 17 In his defense Jesus said to them, “My Father is always at his work to this very day, and I too am working.” 18 For this reason they tried all the more to kill him; not only was he breaking the Sabbath, but he was even calling God his own Father, making himself equal with God.

The paralyzed man at the Bethesda pool needed a change, and Jesus could heal him! Jesus Christ can change our lives, but we have to respond to him in faith.


JUMANNE TAREHE 22 OKTOBA 2019 ASUBUHI                             

10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.
11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.
12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?
13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.
16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. 

Yule mtu aliyepooza katika bwawa la Bethzatha alihitaji badiliko, na Yesu aliweza kumponya! Yesu Kristo anaweza kubadili maisha yetu, lakini tunahitaji kutambua hilo kwa njia ya imani.