Date: 
16-05-2017
Reading: 
JOHN 14:12 (NIV)

WHEN GOD GIVES YOU A NEW SONG

JOHN 14:12 

12 Very truly I tell you, whoever believes in me will do the works I have been doing, and they will do even greater things than these, because I am going to the Father. 13 And I will do whatever you ask in my name, so that the Father may be glorified in the Son. 14 You may ask me for anything in my name, and I will do it.

 

The ministry of signs and wonders is the ministry of God, and He reserves the right to partner with anyone He chooses (Hebrews 2:4). He can partner with someone operating in any of the five-fold ministries; Apostles, Prophets, Pastors, Teachers or Evangelists. He can equally partner with Ushers, Choristers, Instrumentalists, Janitors, etc. When God partners with even an ordinary choir member or instrumentalist, demons will flee! This happened to David when God partnered with him as just a harp player (1 Samuel 16:23). Never look down on yourself! There is yet a song that you can sing to God. God is willing to work with anyone who is willing to cooperate with Him (Rom 8:28b). Are you willing? Are you ready to meet His requirements? Are you asking like some followers of Jesus once asked Him in John 6:28

 

" What shall we do, that we might work the works of God?"

His response to this is in John 14:12;

" Verily, verily, I say unto you, He that believes on me, the works that I do shall he do also; and greater works than these shall he do; because I go unto my Father"

You desire to operate in the miraculous, you must be a person of faith. Why? Faith attracts God into the ordinary situation of life. It brings the divine into contact with the natural. If you have faith, you will have great expectations. If you have faith you won't seek any other alternative to God's intervention. If you have faith, you will not be double minded. If you have faith you will have your new song. Where is your faith? Release it today so that God partners with you in your endeavors! Amen!

 

MUNGU ANAPOKUPA WIMBO MPYA

YOHANA 14:12

12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

 

Maisha ya ishara, maajabu na miujiza ni mpango wa Mungu na Yeye hushirikiana na yeyote yule amchaguaye katika hilo (Ebr 2:4). Hushirikiana na yeyote aliyeitwa katik huduma tano za Kanisa, yaani Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji, na hata Mwalimu. Lakini pia anaweza kuwashirikisha Wahudumu, Wanakwaya, Wanamuziki, Wafagizi, yeyote yule. Na pale Mungu anaposhirikiana na hata mwimbaji tu wa kawaida, mapepo hukimbia na kuwatoka waliopagawa! Hili lilimtokea Daudi! Mungu alishirikiana naye akiwa mpiga kinubi (1Sam 16:23). Kwa hiyo mtu wa Mungu, usijidharau, ukajiona si kitu mbele ya Mungu. Mungu anaweza kumshirikisha yeyote kwenye mipango yake, ili mradi uwe tayari kushirikiana naye (Rum 8:28b). Uko tayari? Umehiyari kushirikiana naye? Uko tayari kukidhi matakwa yake? Au nawe una maswali kama mmoja wa wanafunzi wake aliyeuliza; 

"Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu"(Yn 6:28b)

 

Jibu la Yesu kwako ni hili; 

 

" Amin, Amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye Mimi, Kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba." (Yn 14:12).

 

Unataka kutenda na  kutembea katika nguvu za Mungu kama Yesu, uwe mtu wa imani. Kwa nini? Kwa sababu imani humpendeza Mungu hata kubeba nguvu za Mungu katika maisha ya kawaida. Huunganisha hali ya uungu na hali ya kibinadamu. Ukiwa na imani utakuwa na matarajio makubwa katika maisha! Ukiwa na imani hutatafuta mbadala wa uwepo wa Mungu katika maisha! Ukiwa na imani hutakuwa na njia mbili maishani! Ukiwa na imani Mungu atakupa wimbo mpya maishani mwako. Imani yako iko wapi? Iachilie basi leo uone Mungu akifanya kazi nawe! Amin.