Date: 
13-04-2019
Reading: 
John 12:44-50 (Yohana 12:44-50)

SATURDAY 13TH APRIL 2019 MORNING                             

John 12:44-50 New International Version (NIV)

44 Then Jesus cried out, “Whoever believes in me does not believe in me only, but in the one who sent me. 45 The one who looks at me is seeing the one who sent me. 46 I have come into the world as a light, so that no one who believes in me should stay in darkness.

47 “If anyone hears my words but does not keep them, I do not judge that person. For I did not come to judge the world, but to save the world. 48 There is a judge for the one who rejects me and does not accept my words; the very words I have spoken will condemn them at the last day. 49 For I did not speak on my own, but the Father who sent me commanded me to say all that I have spoken. 50 I know that his command leads to eternal life. So whatever I say is just what the Father has told me to say.”

Jesus is God. He also became a human being and was born in Bethlehem. He lived a perfect life on earth showing us what God is like. Jesus died on the cross bearing our sins and rose again. He did this so that we as sinful humans can be reconciled to God who is Holy.

We will be judged according to our faith or lack of faith in Jesus Christ. You have heard the message. Have you trusted in Jesus Christ as your Lord and Saviour? 

JUMAMOSI TAREHE 13 APRILI  2019 ASUBUHI                          

YOHANA 12:44-50

44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. 
45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka. 
46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 
47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 
48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 
49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 
50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.:

Yesu ni Mungu. Pia alikuja duniani kama binadamu na kuzaliwa kule Bethlehemu. Yesu aliishi maisha matakatifu hapa duniani kumwakilisha Mungu na kutuonyesha jinsi alivyo Mungu. Kisha alitufia msalabani na kufufuka tena. Alifanya hivi kulipa deni la dhambi zetu na kutupatanisha na Mungu ambaye ni mtakatifu.

Watu watahukumiwa kufuatana na imani yao au kutoamini kwao kwa Yesu Kristo. Umeshikia Injili Je! unamtegemea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako? Usichelewe kuamini.