Date: 
15-05-2017
Reading: 
ISAIAH 65:17-18, PSALM 33:8-11 (NIV)

MONDAY 15TH MAY 2017

WHEN GOD GIVES YOU A NEW SONG

ISAIAH 65:17-18,  PSALM  33:8-11 

God gives you a new song when He turns His prophecies into decrees. There is a difference between prophesies and decrees. When you hear "Thus says the Lord", that is a prophesy for which you will have to wait for it to happen, eve pray for its fulfilment. In contrast, when God decides to issue a decree, such as "Let there be light", you will know that you're waiting time is over, as your miracle will manifest immediately (Genesis 1:3). They is no delay because He has decreed it. Psalm 33:8-9 says one reason why the whole earth should fear God is that whenever He speaks, it is done. He gives you a new song when He decides to show you His Almightiness. he did that to Sarah (Genesis 18:11-15). Then He asked, "Is anything too hard for the Lord?" In Luke 1:37 He repeats that nothing is impossible with our God. At Mathew 3:9 Jesus goes further to say this God can produce children out of stones!

 

I say to you, at whatever you are passing through, whatever the specialists have said, cannot hinder my God. Where they are limited, He is not. The resources they lack, He has in abundance. What they do not know, is common knowledge to Him! His word is full of power and gives direction to anything He wants done. 

 

This is why I know that this season, everything standing in your way to laughter and new song in your heart shall give way so that you can burst into a new song, and that song shall be unstoppable. God is saying let there be light, healing, fruitfulness,increase,promotion, victory over enemies and fullness of joy in your life, and shall it be!

MUNGU ANAPOKUPA WIMBO MPYA

ISAYA 65:17-18, ZAB 33:8-11

Mungu akitaka kuibadilisha huzuni yako kuwa furaha, na kukujaza wimbo mpya, huamuru alichosema kitokee! Kuna tofauti kati ya tamko lake, na amri yake. Ukisikia neno lisemalo, "Asema Bwana" ujue hilo ni tamko la Mungu ambalo utalisubiri hata litimie kwa muda alioupanga. Lakini pale anapoamuru, kama vile alivyosema, "Iwepo nuru", (Mwa 1:3) hii haina mjadala, inatokea mara, na utajua muda wako wa kusubiri umekwisha. Haichelewi kwa kuwa ameamuru. Zaburi ya 33:8-9 inasema, sababu mojawapo ya nchi yote imwogope Bwana ni kwa sababu akiamuru kinatokea! Akitaka kukupa wimbo mpya moyoni mwako, huonesha ukuu wake! Alimwonesha Sarah ukuu wake katika Mwanzo 18:11-15 , " Kuna neno  gani lililo gumu la kumshinda Bwana?" Katika Lika 1:37 anarudia kusema tena, "..hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu". Yesu mwenyewe, aliye Neno, anasema katika Mathayo 3:9 kuwa, "..nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahim watoto"

Sasa nakuambia kuwa ukiamini Neno la Mungu, chochote kinachokusumbua, kinachozuia furaha yako, chochote asemacho daktari, hakitamshinda Mungu wetu; hakitadumu, na kitaondoshwa, ili ndani yako furaha yako itimie. Pale wanaposhindwa Yeye anaweza, Pale penye upungufu, Yeye anavyo tele! Kile wasichojua, Kwake ni elimu ya kawaida! Neno lake lina nguvu na linaamuru  chochote kitokee, matakwa Yake!

Ndiyo maana najua kuwa chochote kinachozuia furaha yako na wimbo mpya usipasuke moyo ni mwako, kitaondoka, nawe utajazwa wimbo usiokatika. Mungu anakuambia, kuweko nuru katika maisha yako, ukaponywe, ukazae sana, ukatoe matunda nayo yapate kukaa, ukaongezeke, ukainuliwe, ukatawale malango ya adui zako na maisha yako yake ya furaha, na iwe kama anavyosema!