Date: 
15-03-2019
Reading: 
Hebrews 5:1-10 (Waebrania 5:1-10)

FRIDAY 15TH MARCH 2019

Hebrews 5:1-10 New International Version (NIV)

1 Every high priest is selected from among the people and is appointed to represent the people in matters related to God, to offer gifts and sacrifices for sins. 2 He is able to deal gently with those who are ignorant and are going astray, since he himself is subject to weakness. 3 This is why he has to offer sacrifices for his own sins, as well as for the sins of the people. 4 And no one takes this honor on himself, but he receives it when called by God, just as Aaron was.

5 In the same way, Christ did not take on himself the glory of becoming a high priest. But God said to him,

“You are my Son;

    today I have become your Father.”[a]

6 And he says in another place,

“You are a priest forever,

    in the order of Melchizedek.”[b]

7 During the days of Jesus’ life on earth, he offered up prayers and petitions with fervent cries and tears to the one who could save him from death, and he was heard because of his reverent submission. 8 Son though he was, he learned obedience from what he suffered 9 and, once made perfect, he became the source of eternal salvation for all who obey him 10 and was designated by God to be high priest in the order of Melchizedek.

Footnotes:

Hebrews 5:5 Psalm 2:7

Hebrews 5:6 Psalm 110:4

God appointed Jesus to be the most High Priest who humbly took the task of attonement of our sins by dying on the cross. Even though he was in a position of power, Jesus was humble to his subjects. Let us learn from this, that whatever authority given to us is for serving others humbly.

IJUMAA TAREHE 15 MACHI 2019

WAEBRANIA 5:1-10

1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 
2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu; 
3 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 
4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. 
5 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 
6 kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki. 
7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 
8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 
9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; 
10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. 

Mungu alimteua Yesu kuwa Kuhani Mkuu zaidi ambaye kwa upole alichukua kazi ya kubeba dhambi zetu kwa kufa msalabani. Ingawa alikuwa katika nafasi kubwa ya madaraka, Yesu alikuwa mnyenyekevu kwa watu wake. Hebu tujifunze kutokana na hili, kwamba mamlaka yoyote iliyotolewa kwetu ni kwa kuwahudumia wengine kwa unyenyekevu.