Date: 
20-04-2019
Reading: 
Hebrews 10:8-17 (Waebrania 10:8-17)

SATURDAY 20TH APRIL 2019   MORNING                                           

Hebrews 10:8-17 New International Version (NIV)

First he said, “Sacrifices and offerings, burnt offerings and sin offerings you did not desire, nor were you pleased with them”—though they were offered in accordance with the law. Then he said, “Here I am, I have come to do your will.” He sets aside the first to establish the second.10 And by that will, we have been made holy through the sacrifice of the body of Jesus Christ once for all.

11 Day after day every priest stands and performs his religious duties; again and again he offers the same sacrifices, which can never take away sins. 12 But when this priest had offered for all time one sacrifice for sins, he sat down at the right hand of God, 13 and since that time he waits for his enemies to be made his footstool. 14 For by one sacrifice he has made perfect forever those who are being made holy.

15 The Holy Spirit also testifies to us about this. First he says:

16 “This is the covenant I will make with them
    after that time, says the Lord.
I will put my laws in their hearts,
    and I will write them on their minds.”[
a]

17 Then he adds:

“Their sins and lawless acts
    I will remember no more.”[
b]

Footnotes:

  1. Hebrews 10:16 Jer. 31:33
  2. Hebrews 10:17 Jer. 31:34

Jesus offered Himself as a perfect sacrifice once and for all to atone for the sins of all people in the world. Yesterday we remembered Christ’s suffering and death for us on the cross. He died so that our sins can be forgiven and we can be friends with God.

Thank God for your salvation.

JUMAMOSI TAREHE 20 APRILI 2019 ASUBUHI                  

WAEBRANIA 10:8-17

Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), 
ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. 
10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. 
11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. 
12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 
13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 
14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. 
15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema, 
16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo, 
17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. 

Yesu Kristo alijitoa msalabani kama sadaka kamili. Sadaka ya Yesu Kristo ilitosha kabisa kulipa deni la dhambi za watu wote duniani.

Jana, Ijumaa Kuu, tulikumbuka jinsi Yesu aliteswa na alikufa msalabani  kwa ajili  yetu. Kesho tutasherekea ufufuko wake.

Karibuni katika Ibada zetu tumsifu Mungu.

Mshukuru Mungu kwa Wokovu wako.