Date: 
20-01-2017
Reading: 
Genesis 9:1-3 New International Version (NIV)

FRIDAY 20TH JANUARY 2017 MORNING                                   

Genesis 9:1-3 New International Version (NIV)

God’s Covenant With Noah

1 Then God blessed Noah and his sons, saying to them, “Be fruitful and increase in number and fill the earth. The fear and dread of you will fall on all the beasts of the earth, and on all the birds in the sky, on every creature that moves along the ground, and on all the fish in the sea; they are given into your hands. Everything that lives and moves about will be food for you. Just as I gave you the green plants, I now give you everything.

After destroying evil in the earth with the flood God makes a new covenant with Noah and his family. It is similar to that when God created the world (Genesis 1:27-30). However now God caused the living creatures to be afraid of Mankind. Also People were now given permission to kill animals and eat their meat and not just to eat plants.

Pray that God would help us to be responsible in the way we care for His creation and not just exploit the natural world to fulfill our selfish desires. Let us think how we need to share the world’s resources with other people and take care of the world for future generations.

  

IJUMAA TAREHE 20 JANUARI 2017 ASUBUHI                                  

MWANZO 9:1-3

1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. 
2 Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. 
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. 
 

Baada ya kuangamiza uovu kwa gharika, Mungu alifanya agano jipya na Nuhu na familia yake. Agano kwa sehemu lilifanana na lile Mungu alifanya na watu wa kwanza baada kuumba dunia (Mwanzo 1:27-30). Tofauti ni sasa wanyama wanaogopa binadamu. Pia Mungu aliruhusu binadamu kuchinja na kula wanyama badala ya kula mimea tu.

Mwombe Mungu tuweze kutunza vizuri uumbaji wake kwa faida ya binadamu wote na kwa vizazi vijavyo.