Date: 
11-10-2019
Reading: 
Exodus 14:26-31 (Kutoka 14:26-31)

FRIDAY 11TH OCTOBER 2019  MORNING                               

Exodus 14:26-31 New International Version (NIV)

26 Then the Lord said to Moses, “Stretch out your hand over the sea so that the waters may flow back over the Egyptians and their chariots and horsemen.” 27 Moses stretched out his hand over the sea, and at daybreak the sea went back to its place. The Egyptians were fleeing toward[c] it, and the Lord swept them into the sea. 28 The water flowed back and covered the chariots and horsemen—the entire army of Pharaoh that had followed the Israelites into the sea. Not one of them survived.

29 But the Israelites went through the sea on dry ground, with a wall of water on their right and on their left. 30 That day the Lord saved Israel from the hands of the Egyptians, and Israel saw the Egyptians lying dead on the shore. 31 And when the Israelites saw the mighty hand of the Lord displayed against the Egyptians, the people feared the Lord and put their trust in him and in Moses his servant.

Perseverance results from keeping our focus on God. When we're focused on God our problems are quite small in comparison. Moses' faith caused him to follow through with God's command to challenge Pharaoh to let the Israelites go. Moses' faith allowed him to be more concerned about the wrath of God than the wrath of Pharaoh. We must fear God; not man.


IJUMAA TAREHE 11 MWEZI OKTOBA 2019 ASUBUHI                    

KUTOKA 14:26-31

26 Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao.
27 Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari.
28 Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
29 Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.
30 Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa.
31 Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake.

Tukimwelekea na kumtumaini Mungu yeye anatupa uwezo wa kuvumilia. Tunapomtazama Mungu matatizo yetu huonekana kuwa madogo kulinganisha na nguvu ya Mungu. Imani ya Musa ilimwezesha kufuata agizo la Mungu katika kumwamuru Farao awaruhusu Waisraeli waondoke Misri. Imani yake ilimfanya kuwa na hofu juu ya hasira ya Mungu na siyo ya Farao. Tunapaswa kumwogopa Mungu, na siyo mwanadamu.