Date: 
08-07-2022
Reading: 
Daniel 12:4

Ijumaa asubuhi tarehe 08.07.2022

Danieli 12:4

4 Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

Kijana na uchumi katika zama za utandawazi;

Nabii Daniel alipewa agizo la kuzingatia maelekezo aliyopewa na Mungu katika unabii wake wakati wote ili kuepuka maarifa tofauti ambayo yangempotosha. Lengo ilikuwa kumsaidia aende katika njia sahihi akifanya kazi ya unabii aliyopewa.

Maagizo haya kwa Nabii Danieli ni sawa na leo ambavyo vijana wanaagizwa kulishika neno la Mungu na kudumu katika ibada ili wasipotee. Kijana unaalikwa kudumu katika imani, neno la Mungu likiwa nguzo yako katika kuitika wito wako shambani mwa Bwana. 

Siku njema.