Date: 
02-06-2020
Reading: 
ACTS 2:5-13 (Matendo 2:5-13)

TUESDAY 2ND JUNE 2020  MORNING                                                                                

ACTS 2:5-13 New International Version (NIV)

Now there were staying in Jerusalem God-fearing Jews from every nation under heaven. When they heard this sound, a crowd came together in bewilderment, because each one heard their own language being spoken. Utterly amazed, they asked: “Aren’t all these who are speaking Galileans? Then how is it that each of us hears them in our native language? Parthians, Medes and Elamites; residents of Mesopotamia, Judea and Cappadocia, Pontus and Asia,[b] 10 Phrygia and Pamphylia, Egypt and the parts of Libya near Cyrene; visitors from Rome 11 (both Jews and converts to Judaism); Cretans and Arabs—we hear them declaring the wonders of God in our own tongues!” 12 Amazed and perplexed, they asked one another, “What does this mean?”

13 Some, however, made fun of them and said, “They have had too much wine.”

 

Christ has poured out His Spirit in power, and He is building His church. 

The spread of the gospel didn’t start with a new technique, but with the power of the Holy Spirit. 

In the same way, the power to change a hard heart, and grow the church is not found in a technique, style, method, but in the power of the Holy Spirit through the Word of God.


JUMANNE TAREHE 2 JUNI 2020    ASUBUHI                                

MATENDO YA MITUME 2:5-13

Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.
Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?
Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia,
10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,
11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

Kristo amemtuma Roho wake kwetu katika nguvu, naye analijenga kanisa lake.

Kuenea kwa injili hakukuanza kwa sababu ya mbinu mpya, ila ni kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Vivyo hivyo, nguvu iwezayo kugeuza moyo mgumu, na kulikuza kanisa haipatikani katika ufundi, mitindo, au mbinu, lakini hutoka katika nguvu ya Roho Mtakatifu kwa njia ya Neno la Mungu.