Date: 
08-01-2019
Reading: 
Acts 16:6-12 (Matendo 16:6-12)

TUESDAY 8TH JANUARY 2019 MORNING                           

Acts 16:6-12 New International Version (NIV)

Paul’s Vision of the Man of Macedonia

Paul and his companions traveled throughout the region of Phrygia and Galatia, having been kept by the Holy Spirit from preaching the word in the province of Asia. When they came to the border of Mysia, they tried to enter Bithynia, but the Spirit of Jesus would not allow them to. So they passed by Mysia and went down to Troas. During the night Paul had a vision of a man of Macedonia standing and begging him, “Come over to Macedonia and help us.” 10 After Paul had seen the vision, we got ready at once to leave for Macedonia, concluding that God had called us to preach the gospel to them.

Lydia’s Conversion in Philippi

11 From Troas we put out to sea and sailed straight for Samothrace, and the next day we went on to Neapolis. 12 From there we traveled to Philippi, a Roman colony and the leading city of that district[a] of Macedonia. And we stayed there several days.

Footnotes:

  1. Acts 16:12 The text and meaning of the Greek for the leading city of that district are uncertain.

The Apostle Paul was a very dedicated Missionary and Evangelist. He preached the Gospel in many places and started churches. He wrote many letters to teach, warn, and encourage Christians in various churches. He was sensitive to the guiding of the Holy Spirit and he didn’t do this work in his own strength but by the power and direction of the Holy Spirit.

Do you seek to be guided by the Holy Spirit in all you do? Do you try to share your faith with other people? Resolve that in this New Year 2019 you will start and continue to do God’s work as you are guided by the Holy Spirit.

JUMANNE TAREHE 8 JANUARI 2019 ASUBUHI                          

MATENDO 16:6-12

Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. 
Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, 
wakapita Misia wakatelemkia Troa. 
Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. 
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema. 
11 Basi tukang'oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; 
12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. 

Mtume Paulo alikuwa na bidii sana kufanya kazi ya Mungu kama Misionari na Mwinjilisti. Alisafiri sana kuhubiri Injili na kuanzisha makanisa sehemu mbalimbali. Pia aliandika nyaraka nyingi kwa makanisa kuwafundisha, kuwaonya  na kuwatia moyo. Mtume Paulo aliongozwa na Roho Mtakatifu katika kazi hii yote.

Je! Wewe unatafuta kuongozwa na Roho Mtakatifu kila wakati? Je! Unapata Nafasi kuwashuhudia ndugu, marafiki na majirani kuhusu Neno la Mungu na njia ya wokovu? Amua mwaka huu wa 2019 uanze na uendelea kufanya kazi ya Mungu  jinsi utaongozwa na Roho Mtakatifu.