Date: 
19-01-2019
Reading: 
2Peter 1:16-18

SATURDAY 19TH JANUARY 2019 MORNING 2 PETER 1:16-18

2 Peter 1:16-18 New International Version (NIV)

16 For we did not follow cleverly devised stories when we told you about the coming of our Lord Jesus Christ in power, but we were eyewitnesses of his majesty. 17 He received honor and glory from God the Father when the voice came to him from the Majestic Glory, saying, “This is my Son, whom I love; with him I am well pleased.”[a] 18 We ourselves heard this voice that came from heaven when we were with him on the sacred mountain.

Footnotes:

2 Peter 1:17 Matt. 17:5; Mark 9:7; Luke 9:35

The Apostle Peter knew what he was talking about. He spent three years with Jesus. He saw the miracles and heard Jesus’ teachings. He saw Jesus transfigured on the mountain and heard the voice of God the Father confirming His son. Peter wants his readers to be sure that what he says about Jesus Christ is true.

The Bible is trustworthy and reliable. Read and obey God’s Word in the Bible. 

JUMAMOSI TAREHE 19 JANUARI 2019 ASUBUHI                      

2 PETRO 1:16-18

16 Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. 

17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. 

18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu. 

    

Mtume Petro anataka wasomaji wa waraka huu wawe na uhakika wa maneno yake. Petro alikuwa na Yesu Kristo kwa miaka mitatu, kila siku. Petro alifanya huduma pamoja na Yesu Kristo. Petro alikuwa karibu sana na Yesu. Petro aliona miujiza ya Yesu na kusikia mafundhisho yake. Petro alikuwepo mlimani wakati sura ya Yesu iling’aa na alithibitishwa na sauti ya Mungu Baba toka mbinguni.

Biblia ni Neno la Mungu. Ujumbe wake ni wa uhakika. Tusome na kutii Biblia kila siku.