Date: 
19-06-2017
Reading: 
2 Wakorintho 4:8-10 {2 Corinthians 4:8-10}

UTATU MTAKATIFU: ULIFUNULIWA KWETU TUMSHINDE SHETANI TUKIWA WANA WA MUNGU

2 Wakorintho 4:8-10

8 Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;
9 twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;
10 siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu.

Neno linatuambia kuwa hakuna nafasi ya kushindwa katika maisha yetu hapa duniani. Yesu hakupata kushindwa wala hana mpango wa sisi tushindwe maishani.

Tuna mfano mzuri katika Mtume Paulo, unajua ni nini kilichomwezesha Mtume Paulo kushinda taabu na majaribu aliyokutana nayo? Ni kwa sababu aliweza kusema; "....namjua ninayemwamini ...." (2Timotheo 1:12). Alithibitisha kuwa amekwisha shawishika, na hakuna lolote litakalombadilisha imani yake, awe anazama na meli, awe anapata vipigo, au adha yoyote maishani! Kwamba yote haya hayalingani na uwe utukufu anaoutarajia. Ndani kwake hili limedhihirika! Ni kufunuliwa kwa utukufu wa Mungu mwenye enzi ndani yake, kiasi kwamba hakuna cha kulingana na hicho anachokitarajia! Na kwa jinsi hiyo alipambana na kuvumilia kila jaribu la kila hali, akijua kuwa hawezi kushindwa! 

Yesu hakushindwa kwa kuwa alimkabili Shetani akijijua kuwa ni Mwana wa Mungu aliye hai. Alijua kuwa Mungu yu ndani yake na pamoja naye na alijua angemwezesha kumshinda Shetani.

Sasa uzuri ni kwamba, ukiokoka, Mungu anakujenga kwa upya ufanane na Yesu! Yaani ufikiri na kutenda kama Yesu alivyofanya. Anakujenga na kukutayarisha na kukupa nguvu ya kubambana na Shetani na kumshinda kama vile Yesu alivyopambana na Shetani na kumshinda. 

Hii ina maana kuwa, unapopata ugonjwa na maradhi mwilini mwaka, au pale mpendwa wako anapoumwa unaweza kuukabili ugonjwa na kuuamuru utoke kwa kuwa wewe ni Mwana wa Mungu, na kwamba ndani kwako iko nguvu ya Mungu itendayo kazi (Efe 3:20)

Hata pale hali ya uchumi inapobana na kukutesa, usifadhaike na kukosa usingizi ukiwaza utawezaje kuishi. Kama mwana wa Mungu, unaweza matatizo ya kiuchumi kwa imani na ujasiri ukijua kuwa ndani kwako kuna uwezo ule uwe uliokuwa ndani ya Yesu, alipoongeza vipande vya mkate na samaki na kuwalisha watu elfu tano. 

Kumbuka kuwa hakuna nafasi ya kushindwa katika maisha yako kwa kuwa ndani kwako kuna nguvu ambayo haijapata kushindwa. Ndani kwako kuna nguvu iliyoumba mbingu na nchi na sayari zake. Nguvu iliyolitamka jua, na mwezi na nyota viwepo na vikawa. Kuna nguvu ndani yako inayoponya wagonjwa, kufukuza mapepo, na kufufua wafu! Kuna nguvu ndani yako iliyomkabili Shetani na kumshinda, na kuvunja nguvu ya dhambi. Nguvu lie iliyokuwa ndani ya Yesu imo ndani yako.

Wakristo wengi tunakiri tu wana wa Mungu bila kujua maana yake, maana yake ndiyo hii, ndiyo uhalisia wa kuitwa Mwana wa Mungu.

Kutolijijua hili linatufanya tuishi chini ya viwango1!

 

 

HOLY TRINITY: REVEALED TO US SO THAT WE CAN CONQUER SATAN, KNOWING WE ARE SONS OF GOD

2 Corinthians 4:8-10

We are hard pressed on every side, but not crushed; perplexed, but not in despair; persecuted, but not abandoned; struck down, but not destroyed. 10 We always carry around in our body the death of Jesus, so that the life of Jesus may also be revealed in our body.

The scripture is telling us that, there is no room in our lives for defeat. Jesus was never defeated and He has not planned for us to be defeated.

We have a good example in Paul, do you know why he endured many trials and tribulations and was not defeated? Because he knew whom he believed in (2 Timothy 1:2). He said, "I am persuaded ....it doesn't make any difference whether I face shipwreck or whether I face all kinds of beatings and sufferings all my life".

He said, "None can be compared with what I know. I know there is glory waiting for me. It is inside me. It is the manifestation of God Almighty and nothing can be compared to that glory. I can go through every test, every trial, every circumstance knowing that I cannot be defeated"

Jesus was never defeated because He faced Satan knowing that He was the son of God. He knew that God was in Him and would make Him victorious over Satan. 

God has planned for you to think, walk, talk and act as Jesus did. He has planned for you to face Satan and conquer him in the same power and anointing as Jesus faced and defeated him.

When you face desease and sickness in your body or the body of your friend or loved ones, you can face it and command it to leave knowing that you are the son of God and that the same powerful life-giving flow of God is dwelling in you!

When you are pushed into a corner by mounting financial problems, you do not need to panic or have sleepless nights worrying how you are going to survive. You can face those financial problems with faith and confidence knowing that you are the son of the living God, and knowing that the same powerful force that was in Christ when He multiplied the fish and loaves of bread is in you and will make you victorious!

There's is no room in your life for defeat because there is life within you, that has never been defeated. There is life within you that created the universe....that spoke the sun, the moon and the stars into existence. There is life within you that heals the sick, casts out demons and raises the dead. There is life within you that faced Satan, conquered him and destroyed the powers of sin, sickness and death. The same life giving flow that was in Jesus, is in you! When you were born again, you became a son of the living GOD.

 Most Christians today claim to be sons of God without really knowing what it means to be the son. This above is the reality of being the son of God. 

Living otherwise, is living below standards?