Date: 
13-06-2018
Reading: 
2 Corinthians 5:17 (2 Wakorintho 5:17)

WENESDAY 13th JUNE 2018
BECOMING A NEW PERSON IN CHRIST

2 Corinthians 5:17
“Therefore, if anyone is in Christ, he is a new creation, old things have passed away; behold, all things have become new.”


When you invite Jesus Christ to be your personal Savior and Lord, He actually enters your life, and When He does, He plans to be with you forever. You will never again be alone. When Jesus left the earth after His resurrection, He told His disciples to wait for the “promise” He would send them from His father. This is the Holy Spirit. He has many roles in our lives, but His main role in our lives is to be our “Comforter” and “Encourager” as you embark on your new journey with Christ. As your invited guest, He desires to “settle down” in each room of your “house”. He brings warmth, light, and music. Christ lives in you through the Person of the Holy Spirit.JUMATANO TAHERE 13 JUNI 2018

KUWA MTU MPYA NDANI YA KRISTO

2 Korintho 5:17
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamekwisha, tazama! Yamekuwa mapya.”


Pale unapomkaribisha Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, Yesu huingia hasa katika maisha yako, na anapoingia, hana mpango wa kukaa kwa muda, bali kukaa milele. Hatakuacha pekee tena. Yesu alipopaa baada ya kufufuka, aliwapa wanafunzi wake maagizo ya kusubiri hadi atakapowatumia ahadi itokayo kwa Baba yake! Ahadi hiyo ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ana mambo mengi ya kutufanyia katika maisha yetu, lakini kubwa analotufanyia ni kuwa “Mfariji” na “Anayetutia Moyo” tunapoanza safari ya maisha mapya na Yesu. Na kwa kuwa umemwalika, hupenda kujaza kila chumba cha maisha yako, akikuletea joto la upendo, nuru na tenzi za rohoni. Na hapo ndipo Yesu huishi ndani mwako kupitia Roho Mtakatifu.