Date: 
02-02-2023
Reading: 
1Saweli 12:20-25

Alhamisi asubuhi tarehe 02.02.2023

1 Samweli 12:20-25

[20]Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote.

[21]Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili,

[22]visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.

[23]Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka

[24]Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.

[25]Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.

Kung'aa kwa Yesu Kristo;

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba ya Samweli akiwaaga Israeli baada ya yeye kuzeeka, na Sauli kuingia madarakani. Samweli anawaambia jinsi babu zao walivyokombolewa toka Misri, wakamuasi Bwana ambaye aliwaokoa baada ya kutubu. 

Sasa katika somo la leo asubuhi, Samweli anawaambia wamche Bwana na kumtumikia, wakimsikiliza mfalme wao. Anawaambia wakumbuke Bwana alivyowatendea makuu, ndipo wadumu katika yeye ili wasiangamie.

Bwana alitoa ujumbe wa kumcha yeye kupitia kwa Samweli kwa Taifa lake. Leo tunaitwa kumcha Bwana, tukimwamini Yesu Kristo aliyekufa msalabani kwa ajili yetu ili tusiangamie.

Siku njema.

Heri Buberwa