Date: 
13-05-2017
Reading: 
1Peter 5:10 (NIV)

FORBID EXTENSIONS

1 Peter 5:10

10 And the God of all grace, who called you to his eternal glory in Christ, after you have suffered a little while, will himself restore you and make you strong, firm and steadfast.

The assurance that you have as a believer is that the boat of your life and the endeavours cannot sink. Be assured that every storm, contrary wind and wave that is working against you is only for an appointed time. The Holy Spirit made this clear in 1 Peter 5:10, that

   " But the God of all grace, who has called us into His eternal glory by Christ Jesus, after that you have suffered a while, will make you perfect, establish, strengthen, settle you"

Beloved, don't believe the lie of the devil that things will continue to be worse. They will not. Don't believe that the unpleasant situation you are in will persist. It will not. Every pain, sorrow or distress is for a set time and it will definitely expire. After its expiration, the imperfect shall be perfected, the unstable shall be established, the weak shall be strengthened and there shall be divine settlement. These shall be your portion from now on in Jesus name!

Be blessed!

 

KATAA SHINIKIZO LA MAISHA JUU YAKO

1Petro 5:10

10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.

Mpendwa,  ukiwa mtu wa imani, amini kwamba, kwa hakika maisha yako na mipango uliyowekewa ya maisha haitaharibika kamwe! Lazima uamini kuwa si upepo, wala mawimbi, wala dhoruba inayopingana nawe itafanikiwa, ina kingama name kwa muda tu. Fahamu kuwa Roho Mtakatifu amekwisha sema kuwa,

   "Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, Yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu"

Mpendwa usiamini uongo wa shetani, kwamba mambo yatazidi kuharibika. Haitakuwa hivyo! Usiamini kuwa hali mbaya unayopitia sasa itadumu. Haitadumu! Kila maumivu, huzuni au shinikizo lolote linalokuumiza ni kwa muda tu. Na baada ya muda wake kupita, vilivyotenguliwa vitawekwa sawa, visivyo na uhakika vitathibitishwa, vilivyo dhaifu vitatiwa nguvu na Mungu atakutegemeza. Na hiyo ndiyo itakuwa stahili yako kuanzia sasa na hata milele katika jina la Yesu!

Barikiwa!