Date: 
16-06-2017
Reading: 
1 Wakorintho 12:11-13 {1 Corinthians 12:11-13}

UTATU MTAKATIFU: ROHO YULE YULE ALIYEKUWA NDANI YA KRISTO YUMO KWETU PIA

1 Wakorintho 12:11-13

11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 
12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 
13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 

Je! Neno hili linakushangaza? 

Nasema, Roho Mtakatifu aliyemtia nguvu Bwana Yesu, ndiye huyo huyo anayeishi ndani yetu! Hakuna Roho Mtakatifu wengi, ni mmoja tu.....yule aliyebeba nguvu halisi za Mungu....Ila mwenye huduma, karama na kazi tofauti atupazo sisi. Yule Roho Mtakatifu anayebatiza, ndiye huyo huyo 

 • Anayetupaka mafuta - 1 Yoh 2:20,27
 • Anayetupa kuzaa matunda ya Roho - Gal 5:22-23
 • Ahukumuye ndani mwetu- Yn 16:1,8-11
 • Atufarijiye - Yn 14:16-26
 • Atutiaye nguvu - Mdo 1:8
 • Atupaye karama na vipawa - 1 Wakorintho 12:3-11
 • Atuongozaye - Yn 16:13
 • Atupaye Roho ya hekima na ufunuo - Efe 1:16-17
 • Anatufanya Wapya (Yn 3:3,5)
 • Anatutakasa (Rum 15:16)
 • Anatufundisha (Yn 14:26)
 • Anamshuhudia Kristo kwetu (Yn 15:26)
 • Anatubadilisha tufanane na utukufu wa Kristo (2 Kor 3:18)

Roho yule yule aliyemtakasa Yesu Kristo ndiye huyo akutakasaye na wewe. Huyo Roho atokaye kwa Mungu Baba.

Je! Unajua maana ya hili nisemalo? Yaani, pale unapobatizwa kwa Roho Mtakatifu, na kujazwa na Roho, pale anapojaa na kufurika ndani yako, unakuwa na nguvu na uwezo ule ule uliodhihirika ndani ya Yesu Kristo (Yn 14:12).

Huu ni mpango wa Mungu na kusudi lake kwako. Mungu hakutupangia tuishi kwa woga na kukosa ujasiri....kushindwa na hali ya maisha,....kushindwa na mazingira...kushindwa na mwovu shetani. Mungu hakupanga wewe ushindwe, wewe ni mshindi. Amekupangia wewe uteke nyara na uwe na ushindi daima. 

Mungu alipanga uwe na Roho Mtakatifu yule yule wa Yesu ndani yako, ili ubadilishwe na kufanana na mwanawe Yesu, uweze kudhihirisha ukuu na uwezo alioudhihirisha Yesu akiwa hapa duniani. Kumbuka Bwana Yesu alisema; " Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi" (Yn 20:21). Ndani mwetu iko nguvu, tusibweteke!

HOLY TRINITY: THE SAME SPIRIT THAT ANOINTED JESUS IS THE SAME SPIRIT THAT ANOINTS US.

1 Corinthians 12:11-13

11 All these are the work of one and the same Spirit, and he distributes them to each one, just as he determines.

Unity and Diversity in the Body

12 Just as a body, though one, has many parts, but all its many parts form one body, so it is with Christ. 13 For we were all baptized by[a] one Spirit so as to form one body—whether Jews or Gentiles, slave or free—and we were all given the one Spirit to drink.

Footnotes:

 1. 1 Corinthians 12:13 Or with; or in

You have read the scripture! Now are you ready for this?

Fact is, the Spirit that anointed Jesus is the same spirit that anoints us. There are not two, three or five Spirits, there is only one! That is the Holy Spirit....one true anointing of God.....with many ministries. The same Spirit that baptises also 

 • Anoints (1John 2:20,27)
 • Bears Fruits (Galatians 5:22-23)
 • Convicts (John16:1,8-11)
 • Comforts (John 14:16-26)
 • Empowers (Acts1:8)
 • Gives gifts (1 Corinthians 12:3-11)
 • Guides (John 16:13)
 • Illuminates the mind (Ephesians 1:16-17)
 • Regenerates (John 3:3,5)
 • Sanctifies (Romans 15:16)
 • Teaches (John 14:26)
 • Testifies of Christ (John 15:26)
 • Transforms (2 Corinthians 3:18)

The same Spirit that anointed Jesus is the same Spirit that anoints you. Yes, by God's same Spirit!

Do you realize that means? When you have truly been baptised by the Holy Spirit, and are FILLED...FULL and OVERFLOWING.....you will have the same authority and power that was demonstrated in the life of Jesus! (John 14:12)

This is part of God's plan and purpose for your life. He did not plan for us to go through life fearful....discouraged.....overcome by our circumstances...beaten down by the devil. 

God did not plan any defeats for us. He planned spiritual conquest and and victory!

He planned the same powerful Spirit within us so that we will be conformed and transformed into the image of His Son, whereby we manifest the same dunamis miracle-working power in our lives as Christ demonstrated. Just remember, Jesus said; "....as the Father has sent me, I also send you" (John 20:21). In us there is power, let us not waste it.