Date: 
19-10-2017
Reading: 
1 Thessalonians 4:9-12 NIV (1Wathesalonike 4:9-12)

THURSDAY 19th OCTOBER 2017 MORNING

1 Thessalonians 4:9-12 New International Versions (NIV)

God's love goes hand in hand with hard work.

Now about your love for one another we do not need to write to you, for you yourselves have been taught by God to love each other. 10 And in fact, you do love all of God’s family throughout Macedonia. Yet we urge you, brothers and sisters, to do so more and more, 11 and to make it your ambition to lead a quiet life: You should mind your own business and work with your hands, just as we told you, 12 so that your daily life may win the respect of outsiders and so that you will not be dependent on anybody.

Message

It is a responsibility for each Christian to work hard again with skills. It is not enough to preach to people about the love of God without teaching them to be zealous for God and for handmade work. So it is a serious mistake for a Christian to live a life of begging while that particular person has a sound mind, healthy body and free environment to work. Let's work hard to keep ourselves away from being dependents.

ALHAMISI YA TAREHE 19th OKTOBA 2017 ASUBUHI

1 Wathesalonike 4:9-12

Upendo wa Mungu huenda sambamba na kufanya kazi kwa bidii.

9 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
10 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.
11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; 
12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.

Ujumbe

Ni wajibu wa mkristo mmoja mmoja kufanya kazi kwa bidii tena kwa ueledi. Haitoshi kuwahubiria watu habari za upendo wa Mungu pasipo kuwafundisha kuwa na bidii ya kumpenda Mungu na kufanya kazi za mikono. Kwa hiyo ni kosa kubwa kwa Mkristo kuishi maisha ya kuombaomba hali una akili timamu, viungo vyenye nguvu na mazingira huru. Tufanye kazi kwa bidii ili tusiwe tegemezi.