Date: 
25-06-2018
Reading: 
1 Peter 5:7 (1Petro 5:7)

MONDAY 25th June 2018

"Cast all your anxieties on Him; for He cares about you” (1 Peter 5:7)

When you are in Christ, as you walk with Him in the renewed spirit of your mind, you are reminded to cast all anxieties, whatever their nature, temporal or spiritual, great or small, personal and private, anxieties over your loved ones, your livelihood, your future, your past, your sins.....on Christ.
If anything burdens you and causes you anxiety, cast it upon the Lord! Do not conceal it as if it were something of great value. Do not permit it to oppress you and crush you on the ground. Cast it from you as something which does not concern you. In fact it concerns Him!
“For the Lord cares about you”.
He is truly concerned about you. He feels your anxiety as though it were His own. He would remove your anxiety and give you strength instead.

 



JUMATATU TAREHE 25/06/2018

“..Mkimtwika Yeye fadhaa zenu zote, kwa maana Yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.” (1 Pet 5:7)


Ukiwa ndani ya Yesu, ukitembea naye katika maisha yako katika katika nia mpya ya roho yako, unakumbushwa pia kumtwika Yeye fadhaa zako zote. Si kitu fadhaa hizi ni za namna gani! Ziwe za kiroho au za kimwili, ziwe kubwa au ndogo, ziwe zako binafsi au za jamii, ziwe ni juu ya uwapendao, au ni kwa maisha yako ya sasa, yaliyopita, au ya baadaye! Ziwe ni juu ya dhambi zako! Yesu anakwambia umtwishe Yeye.
Chochote kinachokulemea na kuwa mzigo kwako, mtwike Bwana! Usikifiche kama vile kitu cha thamani kwako. Usikiruhusu kikugandamize hata ushindwe kusogea. Kitoe kisikae kwako! Kiondoe kama vile hakipaswi kuwa kwako na mkabidhi Yeye kinayemhusu! Yesu!
“Mungu anajishughulisha sana na mambo yako”
Amini kwamba, Mungu anakujali sana. Unapohangaika, huwa anayahisi mahangaiko yako kama vile ya kwake binafsi! Anachotaka, ni wewe uje kwake, ayaondoe hayo mahangaiko kwako na kuyachukua Yeye, na badala yake, kukupa uwezo!