Date: 
21-06-2018
Reading: 
1 Corinthians 1:10-17 (1 Wakorintho 1:10-17)

THURSDAY 21st JUNE 2018

1 Corinthians 1:10-17 New International Version (NIV)

A Church Divided Over Leaders

10 I appeal to you, brothers and sisters,[a] in the name of our Lord Jesus Christ, that all of you agree with one another in what you say and that there be no divisions among you, but that you be perfectly united in mind and thought. 11 My brothers and sisters, some from Chloe’s household have informed me that there are quarrels among you. 12 What I mean is this: One of you says, “I follow Paul”; another, “I follow Apollos”; another, “I follow Cephas[b]”; still another, “I follow Christ.”

13 Is Christ divided? Was Paul crucified for you? Were you baptized in the name of Paul? 14 I thank God that I did not baptize any of you except Crispus and Gaius, 15 so no one can say that you were baptized in my name. 16 (Yes, I also baptized the household of Stephanas; beyond that, I don’t remember if I baptized anyone else.) 17 For Christ did not send me to baptize, but to preach the gospel—not with wisdom and eloquence, lest the cross of Christ be emptied of its power.

Footnotes:

  1. 1 Corinthians 1:10 The Greek word for brothers and sisters (adelphoi) refers here to believers, both men and women, as part of God’s family; also in verses 11 and 26; and in 2:1; 3:1; 4:6; 6:8; 7:24, 29; 10:1; 11:33; 12:1; 14:6, 20, 26, 39; 15:1, 6, 50, 58; 16:15, 20.
  2. 1 Corinthians 1:12 That is, Peter

As Christians, we must work together as one body to do God's work. Today we have many denominations with different doctrines. But we all carry Jesus' Christ message, which is one. In Mathew 17 Jesus prayed for his disciples to have unity before he left them. This is an important message to us all today.

ALHAMISI TAREHE 21 JUNI 2018

1 KORINTHO 1:10-17

10 Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na fikira moja na nia moja. 11 Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu. 12 Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, "Mimi ni wa Paulo," mwingine: "Mimi ni wa Apolo," mwingine: "Mimi ni wa Kefa," na mwingine: "Mimi ni wa Kristo,". 13 Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwamba sikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa tu Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jina langu. 16 (Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.) 17 Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.

Kama Wakristo, tunapaswa kufanya kazi pamoja kama mwili mmoja kufanya kazi ya Mungu. Leo tuna madhehebu mengi yenye mafundisho tofauti. Lakini sisi wote hubeba ujumbe wa Yesu Kristo, ambayo ni mmoja. Katika Mathew 17 Yesu aliwaombea wanafunzi wake wawe na umoja kabla ya kuwaacha. Huu ni ujumbe muhimu kwa sisi wote leo.