Date: 
24-03-2023
Reading: 
Yohana 6:32-36

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 24.03.2023

Yohana 6:32-36

32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni.

33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.

34 Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.

35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

36 Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini.

Yesu ni chakula cha uzima;

Baada ya Yesu kuwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, anawaambia waliomfuata kwamba yeye ndiye chakula cha uzima. Huaminika kwamba Yohana aliandika ishara ya kuwalisha watu elfu tano ili iwe rahisi kwake kumtambulisha Yesu kama chakula cha uzima. Yesu anawaambia waliomsikiliza kuwa chakula chenye uzima chatoka mbinguni, na yeye Yesu ndiye chakula hicho.

Habari ya Yesu kuwa chakula cha uzima haikuwa nyepesi, maana watu waliifikiria katika njia ya mwili. Hii inaweza kufananishwa na wale wasiomwamini Yesu bado, ambao hawatambui kwamba Yesu ndiye chakula cha uzima, yaani Yesu ndiye mwokozi wa ulimwengu. Amini kuwa Yesu ndiye mwokozi wa ulimwengu, hii ndiyo kweli.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa