Jumatano asubuhi tarehe 25.01.2023
Yohana 4:1-26
[1]Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza,
[2](lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)
[3]aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.
[4]Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.
[5]Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
[6]Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
[7]Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.
[8]Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.
[9]Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.)
[10]Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
[11]Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
[12]Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
[15]Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.
[16]Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa.
[17]Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume;
[18]kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.
[19]Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!
[20]Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.
[21]Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.
[22]Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
[23]Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
[24]Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
[25]Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
[26]Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
Yesu anaondoa ubaguzi;
Mwanamke Msamaria alimshagaa Yesu kumwomba maji ya kunywa, kwa sababu aliona ajabu yeye Msamaria kuchangamana na Yesu. Mstari wa 9 unaeleza;
Yohana 4:9
[9]Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria)Yesu alijieleza kama Mesiya aliyeleta habari njema kwa ajili ya ulimwengu wote, akijitambulisha kama maji yaliyo hai.
Yesu na mwanamke Msamaria ni habari inayotukumbusha kuwa yeye (Yesu) ni maji yaliyo hai. Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
Yesu alionesha kwa vitendo kuwa yeye alikuja kwa ajili ya wanadamu wote pale alipompa mwanamke msamaria habari njema. Alionesha kutobagua maana aliongea na Msamaria. Tuwe na tabia ya Yesu ya kuwapenda watu wote, kama yeye alivyoleta habari njema kwa wote.
Siku njema.