Date: 
25-07-2022
Reading: 
Yohana 15:9-13

Jumatatu asubuhi tarehe 25.07.2022

Yohana 15:9-13

[9]Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.

[10]Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

[11]Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

[12]Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.

[13]Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

Amri mpya nawapa, Mpendane.

Yesu alifundisha kuwa yeye ni mzabibu, sisi ni matawi, na Baba yake ndiye mkulima. Mkulima anamiliki shamba la mizabibu, na mizabibu ina matawi. Tawi lazima liwe kwa mzabibu ili lizae matunda. Hiyo inamaanisha sisi kukaa kwa Yesu ili kudumu katika wokovu.

Tunapodumu katika wokovu, ndipo Yesu katika somo la leo asubuhi anatuambia kwamba kuwa matawi hakutoshi, bali tukishakaa ndani yake, tupendane sisi kwa sisi. Mstari wa tisa unatusisitiza kupendana kama Yesu alivyotupenda na kufa kwa ajili yetu. 

Tunakumbushwa kupendanana wenyewe kama tunavyoamriwa na Kristo maana hatuwezi kuwa watu wake bila kufuata amri zake. Tukizishika amri zake tutakaa katika pendo lake, leo na siku zote.

Uwe na wiki njema yenye upendo wa Kristo.