Date: 
11-06-2022
Reading: 
Yohana 14:16-17

Jumamosi asubuhi tarehe 11.06.2022

Yohana 14:16-17

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Roho Mtakatifu njoo kwetu;

Yesu aliweka ahadi ya kutuachia Roho Mtakatifu ambayo aliitimiza. Katika Injili ya Yohana Yesu anasema lazima Roho huyu tumtambue kwa kukaa ndani yetu. Asipokaa ndani yetu hatuwezi kumtambua, hivyo hawezi kutusaidia.

Hapa lipo swali la kujiuliza;

Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu?

Tunamtambua?

Ukiendelea kusoma (18) Yesu anasema sitawaacha yatima. Kumbe ukiwa hauna Roho Mtakatifu ndani yako unakuwa yatima.

Siku njema.