Date: 
30-08-2022
Reading: 
Yeremia 49:14-16

Jumanne asubuhi tarehe 30.08.2022

Yeremia 49:14-16

[14]Nimepata habari kwa BWANA, 

Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, 

Akisema, Jikusanyeni, mkaujie, 

Mkainuke kwenda vitani.

[15]Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa, 

Na kudharauliwa katika watu.

[16]Katika habari za kuogofya kwako, 

Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, 

Wewe ukaaye katika pango za majabali, 

Ushikaye kilele cha milima; 

Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, 

Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.

Iweni wanyenyekevu;

Yeremia alitumwa kupeleka ujumbe Edomu ambayo watu wake walikuwa wamemwacha Bwana. Mstari wa 16 unaonesha walivyojaa kiburi wakijidanganya na kazi zao. Mstari unaofuata unawaonya;

Yeremia 49:17
[17]Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.

Kanisa na jamii yetu kwa ujumla tunawajibika kumcha Bwana. Tusijae viburi na kuona tumefanikiwa kwa sababu ya uwezo wetu. Bwana hapendi tukijikweza kwa namna hiyo. Tutambue kuwa Mungu ndiye muumbaji anayetuwezesha katika yote, hivyo tunyenyekee mbele zake tukimtumikia kwa uaminifu.

Siku njema.