Date: 
30-06-2022
Reading: 
Yeremia 11:1-5

Alhamisi asubuhi tarehe 30.06.2022

Yeremia 11:1-5

1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,

2 Yasikieni maneno ya maagano haya; ukaseme na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu;

3 ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya,

4 niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;

5 ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi ijaayo maziwa na asali, kama ilivyo leo hivi. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee Bwana.

Wito wa kuingia ufalme wa Mungu;

Nabii Yeremia anapokea ujumbe toka kwa Bwana, kwamba na alaaniwe yeyote asiyeyasikia maneno na maagano ya Bwana. Mungu aliwatoa Israeli Misri utumwani, lakini anawalaani wote ambao hawakumsikia hata baada ya kufika nchi ya ahadi. 

Yesu aliyetuita na kutuokoa anatualika kumwamini, kuishi maisha ya kusikia neno lake na kumfuata. Ni kwa njia hiyo tu tutaweza kuingia katika ufalme wake. Chukua hatua ya imani ili kuingia katika ufalme wake.

Siku njema.