Date: 
31-01-2022
Reading: 
Wathesalonike 5:7-11

Jumatatu asubuhi tarehe 31.01.2022

1 Wathesalonike 5:7-11

7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.

9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;

10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.

11 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.

Tunalindwa na nguvu za Mungu;

Mtume Paulo anaandika akionesha kuwa wakati wengine wakitenda mema, wapo wafanyao uovu. Anatoa mfano wa wengine walalao usiku, wakati huo wapo wanaolewa usiku huohuo. Mtume Paulo anaonesha kuwa siyo lengo la Mungu tuwe dhambini. Ndiyo maana Yesu Kristo alikufa na kufufuka ili tuokolewe.

Tutafakari tunatumiaje wakati wetu hapa duniani tunapomtumikia Mungu. Tunatenda mema au mabaya? Tunawajibika kutenda mema, ndiyo lengo lake Mungu wetu. Tutaweza kushinda dhambi tukitenda mema kwa kuitegemea neema, maana tunalindwa na nguvu za Mungu. 

Tunakutakia wiki njema, ulindwe na nguvu za Mungu.