Date: 
12-01-2023
Reading: 
Warumi 4:9-10

Alhamisi asubuhi tarehe 12.01.2023

Warumi 4:9-12

[9]Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.

[10]Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

[11]Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;

[12]tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa.

Ubatizo wetu;

Ibrahimu anatajwa kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo yake. Alimwamini Mungu na kumsikia, hivyo akawa na matendo mema mbele za Mungu. Tunaona hivi kwa kurejea historia tunapokumbuka alivyoitika wito wa kuhama nchi yake. Pia tunavyokumbuka jinsi alivyomtii Bwana ikiwemo kuwa tayari kumtoa Isaka kama sadaka kwa Bwana. Utii wake na Imani ulitosha kwake kuhesabiwa haki.

Ubatizo umetufanya wana wa Mungu. Leo tunakumbushwa kumtii Mungu ambaye ametuita kwa njia ya Ubatizo. Tunakumbushwa kuwa na maisha ya utii kwa Mungu wetu, tumsikie na kumtumikia kwa uaminifu maana yeye ndiye aliyetuita. Utii wetu kwa Mungu utatupa hatma njema. 

Siku njema.