Date: 
05-04-2022
Reading: 
Walawi 16:29-25

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 05.04.2022

Mambo ya Walawi 16:20-28

20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.

21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.

22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.

23 Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo;

24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu.

25 Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu.

26 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago.

27 Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao.

28 Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia maragoni.

Yesu Kuhani mkuu;

Somo la leo asubuhi ni utangulizi wa somo la mahubiri la Jumapili iliyopita, ambapo tunasoma juu ya Haruni kama Kuhani alivyoingia hekaluni na kufanya ibada ya sadaka ya kuteketezwa, na baadaye upatanisho. Watu walipatanishwa na Mungu kupitia ibada aliyoifanya Kuhani.

Sisi tumepatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani. Hatuhitaji kuchinja mbuzi wala kondoo kwa upatanisho. Wajibu wetu ni kuishi tukitenda yatupasayo, ili neema hii ya upatanisho isiondoke kwetu. 

Usiku mwema.