Date: 
13-01-2023
Reading: 
Waefeso 2:5-8

Ijumaa asubuhi tarehe 13.01.2023

Waefeso 2:5-8

[5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

[6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

[7]ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

[8]Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

Ubatizo wetu;

Tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, tulihuishwa pamoja na Kristo. Yaani tulipokuwa dhambini, Yesu alikuja kutuokoa. Hiyo ni neema ya Mungu ambayo aliidhihirisha Yesu Kristo, kwamba kwa neema yake alituokoa. Hivyo hatujaokolewa kwa uwezo wetu, wala matendo yetu, bali kwa neema tu. 

Kama tulivyoona, neema ya Mungu ndiyo imetuokoa. Kumbe tusiichezee neema hii. Ubatizo ni neema, maana kwa njia ya ubatizo tunampokea Yesu na kusamehewa dhambi zetu. Sasa kama tulivyompokea Yesu tulipobatizwa, tudumu katika neema hii ya ubatizo tukitenda mema, ili tuurithi uzima wa milele.

Siku njema