Hii ni Kwaresma
Jumamosi asubuhi tarehe 01.04.2023
Waebrania 6:16-20
16 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.
17 Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;
18 ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
19 tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,
20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
Yesu ni mpatanishi
Asubuhi hii tunasoma juu ya uhakika wa ahadi ya Mungu katika kumkomboa mwanadamu. Ahadi ya Mungu ni zaidi ya kiapo chochote, maana kiapo hutimizwa kulingana na uwezo wa mtu, mazingira na utashi. Lakini Yesu Kristo aliupatanisha ulimwengu na Mungu kwa ukamilifu, tofauti na viapo vya watu hapa duniani. Ahadi yake ya kutuokoa ni kweli.
Mstari wa 20 unamtaja Yesu Kristo kama kuhani Mkuu. Mungu alitimiza ahadi yake ya kuokoa ulimwengu kwa kumtuma Yesu Kristo duniani, na ahadi hii ilitimia. Ndiyo maana ujumbe wa asubuhi hii ni uhakika wa ahadi ya Mungu. Uhakika ni kuwa Yesu ametuokoa kwa kufa msalabani. Tutubu na kurejea kwake.
Jumamosi njema
Heri Buberwa