Date: 
07-03-2022
Reading: 
Waebrania 2:7-18

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 07.03.2021

Waebrania 2:17-18

17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.

18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.

Tukimtegemea Bwana Tutashinda majaribu;

Mwandishi anamuongelea Yesu Kristo aliyetoka mbinguni akaja duniani kama Mungu kweli na mwanadamu kweli, akiwa kuhani mkuu katika Bwana ili kuwapatanisha watu na Mungu. Na katika hilo, alijaribiwa akashinda majaribu, ambapo huwasaidia wamwaminio kushinda majaribu.

Ujio wa Yesu ulikuwa ni kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu. Kujaribiwa kwake kwa siku arobaini na kushinda majaribu lilikuwa ni tangazo kwa ulimwengu, kuwa yeye ni mshindi, atakayetuwezesha kushinda. Tufahamu ya kuwa tunaweza kushinda majaribu ya kila siku kwa nguvu ya neno lake, na kwa neema yake. Mtegemee Bwana ushinde majaribu.

Nakutakia wiki njema yenye kushinda majaribu.