SAFARI YA UINJILISTI YA KWAYA YA AGAPE EVANGELICAL SINGERS MJINI ARUSHA USHARIKA WA ENABOISHU TAREHE 07 – 10 /08/2014

dep2

Wanakwaya wa Agape Evangelical Singers wakiwa wanaondoka Kanisa kuu Azania front

kuelekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere tayari kwa safari

ya uinjilisti mkoani Arusha.

dep1

Waimbaji wa Kwaya Agape Evangelical Singer wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya

kuwasili uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa kuanza safari ya kwenda

MkoaniArusha kwa ziara ya siku tatu.

mbug1

Baadhi ya waimbaji wa Agape Evangelical Singers wakiwa katika picha ya pamojamara baada ya

kuwasili mbuga ya wanyama Tarangire siku ya pili ya safari yao Mkoani arusha.

mbug2

_________________________________________________________________________________

Siku ya pili wanakwaya waliingia katika mazoezi ya pamoja ikiwa ni pamoja

nampira wa miguu, ambapo ilichezwa mechi kati ya wanakwaya wa Agape na

wenyeji wao kwaya ya uinjilisti Loruvan ya Usharika wa Enaboishu. Mazoezi

ya kupasha motoviungo kabla ya mechi ya mpira wa miguu iliyohusisha

wanawake na wanaume wakwaya ya Agape na Loruvan.

mech1

mech2

Kipa mashuhuri Mr. Peter Mlagha wa Agape akiwa anadaka mpira ulioelekezwa

golini kwake wakati wa mechi hiyo.

mech3

Beki namba tatu mashuhuri wa Agape Miss. Joseline Lutahakana akimnyang’anya

mshambuliaji hatari wa Loruvan Mr.Hezron Mashauri.

mech4

Mshambuliaji machachari wa Agape Mr. Moses Kombe akimnyanganya mpira

beki wa Loruvani katika jitiada za kutafuta goli la pili.

imba1

Agape wakimsifu Mungu katika Ibada ya shukrani, wakiwasindikiza marafiki

zao Kwaya ya uinjilisti Loruvan katika usharika wa Enaboishu Mjini Arusha.

imba2

Agape na Uinjilisti wakiimba kwa pamoja mara baada ya kutoka katika Ibada

katika Usharika wa Enaboishu.

imba4

Agape wakiimba wimbo wa Kizaramo, pwani na kigogo katika tamasha la

kitamaduni walilo onesha kwaya ya Agape katika usharika wa Ngateu mtaa wa

Kiranyi.

imba5

imba6

Umati wa washarika wakifuatilia tamasha la Uimbaji wa Ngateu Mtaa wa

Kiranyi.

imba7

Kwaya ya Agape na Uinjilisti Loruvani wakiwa katika picha ya pamoja mara

baada ya kumaliza tamasha la uimbaji lililofanyika Dayosisi ya Kaskazini Kati

Mkoani Arusha.