SAFARI YA UINJILISTI YA KWAYA YA AGAPE EVANGELICAL SINGERS MJINI ARUSHA USHARIKA WA ENABOISHU TAREHE 07 – 10 /08/2014
Wanakwaya wa Agape Evangelical Singers wakiwa wanaondoka Kanisa kuu Azania front
kuelekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere tayari kwa safari
ya uinjilisti mkoani Arusha.
Waimbaji wa Kwaya Agape Evangelical Singer wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kuwasili uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa kuanza safari ya kwenda
MkoaniArusha kwa ziara ya siku tatu.
Baadhi ya waimbaji wa Agape Evangelical Singers wakiwa katika picha ya pamojamara baada ya
kuwasili mbuga ya wanyama Tarangire siku ya pili ya safari yao Mkoani arusha.
_________________________________________________________________________________
Siku ya pili wanakwaya waliingia katika mazoezi ya pamoja ikiwa ni pamoja
nampira wa miguu, ambapo ilichezwa mechi kati ya wanakwaya wa Agape na
wenyeji wao kwaya ya uinjilisti Loruvan ya Usharika wa Enaboishu. Mazoezi
ya kupasha motoviungo kabla ya mechi ya mpira wa miguu iliyohusisha
wanawake na wanaume wakwaya ya Agape na Loruvan.
Kipa mashuhuri Mr. Peter Mlagha wa Agape akiwa anadaka mpira ulioelekezwa
golini kwake wakati wa mechi hiyo.
Beki namba tatu mashuhuri wa Agape Miss. Joseline Lutahakana akimnyang’anya
mshambuliaji hatari wa Loruvan Mr.Hezron Mashauri.
Mshambuliaji machachari wa Agape Mr. Moses Kombe akimnyanganya mpira
beki wa Loruvani katika jitiada za kutafuta goli la pili.
Agape wakimsifu Mungu katika Ibada ya shukrani, wakiwasindikiza marafiki
zao Kwaya ya uinjilisti Loruvan katika usharika wa Enaboishu Mjini Arusha.
Agape na Uinjilisti wakiimba kwa pamoja mara baada ya kutoka katika Ibada
katika Usharika wa Enaboishu.
Agape wakiimba wimbo wa Kizaramo, pwani na kigogo katika tamasha la
kitamaduni walilo onesha kwaya ya Agape katika usharika wa Ngateu mtaa wa
Kiranyi.
Umati wa washarika wakifuatilia tamasha la Uimbaji wa Ngateu Mtaa wa
Kiranyi.
Kwaya ya Agape na Uinjilisti Loruvani wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kumaliza tamasha la uimbaji lililofanyika Dayosisi ya Kaskazini Kati
Mkoani Arusha.