Date: 
03-08-2018
Reading: 
Philippians 1:27-30 ( Wafilipi 1:27-30)

FRIDAY 3RD AUGUST 2018 MORNING                                  

Philippians 1:27-30 New International Version (NIV)

Life Worthy of the Gospel

27 Whatever happens, conduct yourselves in a manner worthy of the gospel of Christ. Then, whether I come and see you or only hear about you in my absence, I will know that you stand firm in the one Spirit,[a]striving together as one for the faith of the gospel 28 without being frightened in any way by those who oppose you. This is a sign to them that they will be destroyed, but that you will be saved—and that by God.29 For it has been granted to you on behalf of Christ not only to believe in him, but also to suffer for him, 30 since you are going through the same struggle you saw I had, and now hear that I still have.

Footnotes:

  1. Philippians 1:27 Or in one spirit

The Apostle Paul wrote this letter to the church at Philippi to encourage Christians there. He knows about some of their struggles. He wants to encourage them to stand together and to support one another.

Jesus did not promise that it would be easy to be a Christian, but He promised to be with us. Let us not give up when the going is tough. Let us trust in God, encourage, and pray for one another.

IJUMAA TAREHE 3 AGOSTI 2018 ASUBUHI                          

FILIPI 1:27-30

27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; 
28 wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu. 
29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; 
30 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.

Mtume Paulo akiwaandikia Wakristo kule Filipi anawatia moyo. Anajua wanapata mateso kama hata yeye anayvopata. Anawatia moyo wasikate tamaa. Washikamane na kupendana, na kufanya kazi ya Mungu pamoja.

Wakristo wa leo tufuate ushauri huu. Yesu hakuahidi kwamba maisha ya Kikristo yatakuwa rahisi. Lakini aliahidi kuwa nasi. Pia umoja ndani ya Kanisa ni muhimu. Tusiwe wa pweke,  bali tuombeane na kusaidiana.