MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 28 MEI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI USIKIE KUOMBA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na cheti.

3. Leo kutakuwa na Kipindi cha maombi na maombezi saa10.00 jioni yatakayoongozwa na mtumishi Tito Mpesa toka KKKT Kigogo. Aidha siku ya  alhamisi kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi kuanzia saa 11.30 jioni. Wote mnakaribishwa.

4. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni

5. Jumapili ijayo tarehe 04/06/2017 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini.Watakao hitaji huduma hii wafike ofisi ya Mchungaji.

6. Jumapili ijayo tarehe 04/06/2017 katika ibada ya pili saa 3.30 familia mbili zitamshukuru Mungu.

  • Familia ya Bwana Francis Mugizi Ndamagi atamshukuru Mungu kwa kumtia nguvu tangu Mke wake Mpenzi Hilda Michael Mollel aliyetwaliwa na Bwana 30/04/2017 pamoja na mambo mengi aliyomtendea.
  • Neno: Zaburi 23:1-6,Wimbo: TMW 309 (Karibu na wewe)
  • Bwana Ipyana Stephano Mwangosi naye atamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyomtendea ikiwa ni pamoja na kumpa uponyaji, kumuwezesha Mtoto wake Rachel kumaliza Kidato cha Sita salama.

Neno: Zaburi 125,  Wimbo: Kwaya ya vijana (Namshukuru Mungu)  

7. Wale wote waliojiandikisha kwa ajili ya safari ya kwenda Messiah Marekani wanaombwa kufika ofisi ya usharika kupata barua ya mwaliko ili kufanya maandalizi ya Visa.

8. Kwaya Kuu ya Usharika itakuwa na mkutano Mkuu wa mwakautakaofanyika tarehe 03 Juni, 2017 katika Hoteli ya Sembata Kinyerezi. Waimbaji wote wa Kwaya Kuu na Walezi wanaombwa kuhudhuria mkutano huu muhimu. Washarika tuwaombee.

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Watatangaziana
  • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
  •  
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Askf na Mama Alex Malasusa
  •  
  • Tabata: Watatangaziana
  •  
  • Mjini kati: Kwa Mama Hilda Rwanshane
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bw. na Bibi David Korosso

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.