Date: 
30-09-2025
Reading: 
Mithali 23:22-25

Jumanne asubuhi tarehe 30.09.2025

Mithali 23:22-25

22 Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.

23 Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.

24 Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.

25 Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.

Tuwapende na kuwajali watoto katika Bwana;

Mfalme Suleimani anatoa usia wa kumsikiliza baba na mama. Hapa anafundisha heshima kwa wazazi wetu. Katika heshima hiyo anaendelea kufundisha juu ya hekima na mafundisho na ufahamu. Suleimani anasema baba wa mwenye haki atashangilia, na mwenye mtoto aliyejaa hakima atamfurahia mwanae.

Msingi wa Suleimani ni kwa watoto kuwaheshimu wazazi wao. Ndiyo maana mwishoni Suleimani anasema wazazi wakiwa na mtoto mwenye heshima hufurahi. Ni wito wangu kwako, kwamba tuwalee watoto katika njia ya Kristo ili kuijenga jamii yanye heshima, maana itakuwa na watu wanaomcha Bwana. Tuwafundishe watoto kusikiliza, kuheshimu, kutii, ili wawe na ustawi mzuri. Amina

Jumanne njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com