Date:
08-07-2025
Reading:
Methali 10:4-6
Jumanne asubuhi tarehe 08.07.2025
Mithali 10:4-6
4 Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
Msingi wa uongozi bora;
Kijana Mkristo ni chachu ya maendeleo;
Sura ya 10 ya kitabu cha Mithali huangazia tofauti ya wenye haki na waovu, kwa kuonesha maumivu ya njia husika (haki au uovu) katika njia ya imani. Sura huonesha umuhimu wa hekima, uaminifu na umakini katika kupambanua yapasayo kutenda. Sura ya 10 pia hufundisha juu ya mahusiano ya familia, matumizi ya maneno, kuacha uvivu na baraka zitokazo kwa Bwana kwao wamchao.
Somo la asubuhi hii ni sehemu ya sura ya 10, ambapo katika kuifuata haki ya Mungu na kutenda inavyopasa, tunasoma juu ya kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu. Somo linaonesha kwamba mafanikio huja kwa bidii ya kazi, kinyume cha hapo ni aibu na njaa. Mungu anaahidi baraka kwa wote wafanyao kazi kwa bidii wakimtanguliza yeye. Tufanye kazi kwa bidii tukisali bila kukoma, ili tufanikiwe katika Bwana. Amina
Siku njema
Heri Buberwa